Mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo -DRC, Mtanzania Thomas Ulimwengu hatimae amerejea Tanzania ili kuanza upya maisha ya soka la ushindani ndani ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara.
Mchezaji huyo ametambulishwa jana kama mchezaji mpya wa Singida Fountain Gate.
Ulimwengu anarejea kucheza soka Tanzania baada ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kwa miaka 13. Ulimwengu amewahi kucheza soka Tanzania kwa kipindi kifupi cha mwaka 2009-2010.
Baada ya hapo Ulimwengu alijiunga na vilabu vya TP Mazembe (2011-2016), AFC Eskilstuna ya Sweden (2017), Sloboda Tuzla ya Bosnia (2017-2018), Al Hilal ya Sudan (2018), JS Saoura ya Algeria (2019) na TP Mazembe tena (2020-2022).
0 Comments